Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Khalfany Haule amewataka Wananchi kutumia vizuri mvua za masika zilizoanza kunyesha kupanda mazao yanayokomaa kwa muda mfupi mfano Mihogo,Viazi,Mtama,Maharage,Alizeti na mengineyo ili kuhakikisha kila kaya inauhakika wa chakula.
Dc ametoa ushauri huo baada ya muda mrefu kuwa na upungufu wa mvua na hivyo kupelekea janga la njaa katika Wilaya yetu na hivyo kuzorotesha maendeleo. Amewataka Wananchi wautumie vizuri Msimu huu wa mvua kwa kilimo kwa maendeleo yetu sote.
Mhe. Dc anamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ruzuku ya mbolea na mbegu za Alizeti zinazopatikana Murangi, Mugango ,Masinono na Saragana kwa bei ya Tshs 5,000/= kwa kilo pamoja na Mbolea za kupandia na kukuzia za OCP kwa bei ya Tshs 70,000/= kwa mfuko wa Kg 50. Pia Viuatilifu vya kutosha vinapatikana kwa Maafisa Kilimo wa Kata , Vijiji na AMCOS zote 34 zilizoko Halmashauri ya Wilaya Musoma.
Imetolewa na: Kitengo cha Habari-Musoma Dc
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa