Thursday 8th, January 2026
@KIJIJI CHA KURWAKI, MUGANGO
Kamati ya Maafa ya Wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imefanya tathmini ya maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyeesha tarehe 29 Disemba, 2025, katika Kijiji cha Kurwaki kilichopo Kata ya Mugango.
Mvua hiyo ilisababisha athari mbalimbali ikiwemo kubomoka kwa kuta za nyumba na baadhi ya nyumba kubomoka kabisa, hali iliyowalazimu waathirika kupata hifadhi ya muda kwa ndugu na majirani zao.
Akizungumza wakati wa zoezi la tathmini, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu Magange H. Mwita, ametoa pole kwa wananchi waliopatwa na maafa hayo. Aidha, amewataka viongozi wa Serikali ya Kijiji kuendelea kuwaelimisha wananchi kuchukua tahadhari zinazostahili katika kipindi hiki cha mvua ili kuepusha madhara zaidi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa