Sunday 21st, December 2025
@HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA
UZINDUZI WA KAMPENI YA MWEZI WA AFYA NA LISHE KWA MTOTO – DESEMBA 2025
Kampeni ya Mwezi wa Afya na Lishe kwa Mtoto hufanyika kitaifa mara mbili kwa mwaka, mwezi Juni na Desemba. Kwa mwaka huu kampeni ya mwezi wa Desemba 2025 itaanza rasmi tarehe 1 hadi 31 Desemba 2025.
Kampeni hii inalenga kuboresha afya na ustawi wa watoto nchini kwa kutoa huduma muhimu za kinga na ufuatiliaji wa hali ya lishe.
Huduma zitakazotolewa
Kipindi hiki cha kampeni, watoto walio katika makundi lengwa watapata huduma zifuatazo:
Utoaji wa matone ya Vitamini A
Kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 59.
Utoaji wa dawa za minyoo
Kwa watoto wenye umri wa miezi 12 hadi 59.
Upimaji wa hali ya lishe
Kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 59, ili kubaini mapema changamoto za udumavu, ukondefu au uzito pungufu.
Huduma za kampeni zitatolewa kupitia njia mbalimbali ili kuwafikia watoto wote:
Vituo vya kutolea huduma za afya
Huduma za kaya kwa kaya (house-to-house)
Kupitia SALiKi
Huduma mkoba kwenye maeneo ya mikusanyiko, ikijumuisha pia nyumba za ibada
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa