Askari Polisi kutoka Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto, wakishirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, wametoa elimu ya ulinzi na usalama wa mtoto kwa wanafunzi wa Zahanati ya Bukima na Shule ya Sekondari Bukima iliyopo Kata ya Bukima pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Burungu katika Kata ya Bukumi.
Elimu hiyo ilihusisha masuala muhimu yafuatayo:
Ukatili wa Kijinsia (GBV) – aina za ukatili, kutambua viashiria, madhara, na taratibu za kuripoti matukio.
VVU/UKIMWI – njia za maambukizi, namna ya kujikinga, na kuepuka unyanyapaa katika jamii.
Haki za Binadamu na Haki za Mtoto – uelewa wa haki za msingi, wajibu wa wanafunzi, na mbinu za kujilinda.
Huduma za Dawati la Jinsia na Watoto – kupokea taarifa za ukatili, usiri wa taarifa, msaada wa kisheria, na ushauri nasaha.
Nafasi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii – utoaji wa elimu ya ulinzi, ufuatiliaji wa matukio, kuratibu huduma za msaada wa kijamii, na kuhamasisha jamii kutokomeza ukatili.
Shughuli hiyo ililenga kuongeza uelewa wa wanafunzi kuhusu kutambua, kuzuia na kuripoti matukio ya ukatili, pamoja na kujua mahali pa kutafuta msaada kupitia Dawati la Jinsia na Watoto na Idara ya Maendeleo ya Jamii.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa