Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Charles Magoma leo Oktoba 31, 2024 imetembelea miradi ya SWASH ya ujenzi wa vyoo katika shule za Msingi zilizopo katika Halmashauri yetu.
Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa matundu 15 ya vyoo vya shule ya Msingi Wanyere B, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Erick Mosha amesema walipokea kiasi Cha Tshs 43,769,154.07 mnamo Tarehe 14/11/2023 na mpaka sasa wameshatumia kiasi Cha Tshs 23,776,631.57 Kwa kufikia hatua ya upauaji.
"Ucheleweshaji wa mradi wetu kutokamilika ni kutokana na ukosekanaji wa Vifaa vya ujenzi vinavyonunuliwa kupitia mfumo wa manunuzi(nest) ambao wazabuni walioomba zabuni bei zao za utoaji huduma ziko juu ukilinganisha na bei ya soko na hivyo kupelekea zabuni hizo kutangazwa tena". Mwl. Erick Mosha ( Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Wanyere B) akiwaambia wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango.
Wajumbe wa Kamati wametembelea pia shule ya Msingi Seka,Kurugongo na Chimati ambao wote wako katika hatua ya upauaji. Kamati imewaagiza wasimamizi wa miradi hii kuwa imetoa muda wa wiki mbili Kwa miradi yote kukamilika kwani hawana sababu ya Msingi ya kuchelewesha ukamilishwaji wa miradi hiyo
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa