Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imetekeleza mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo Waheshimiwa Madiwani, yanayofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 12 hadi 14 Januari, 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Musoma.
Mafunzo haya yamelenga kuwaongezea uelewa na uwezo Waheshimiwa Madiwani katika kulisimamia Baraza la Madiwani na Halmashauri kwa ujumla, hususan katika utekelezaji wa majukumu yake ya kisheria na kiutawala kwa manufaa ya wananchi.
Jumla ya Waheshimiwa Madiwani 28 wanashiriki mafunzo haya, ambapo 21 ni madiwani kutoka kila kata za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na 07 ni madiwani wa viti maalumu.
Katika mafunzo hayo, mada mbalimbali zinawasilishwa zikiwemo uongozi na utawala bora, wajibu, majukumu, haki na stahiki za diwani, pamoja na usimamizi na udhibiti wa fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mada nyingine muhimu ni pamoja na sheria zinazosimamia uendeshaji wa shughuli za Serikali za Mitaa, muundo, majukumu na madaraka ya Serikali za Mitaa, maadili ya Waheshimiwa Madiwani, pamoja na uendeshaji wa vikao na mikutano katika mamlaka za Serikali za Mitaa.
Kupitia mafunzo haya, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma inalenga kuimarisha utendaji kazi wa Waheshimiwa Madiwani ili kuongeza ufanisi, uwajibikaji na uwazi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa