Leo Oktoba 9, 2024 katika Ukumbi wa Hospitali ya Wilaya ya Musoma, Wataalamu na Wasimamizi wa Mikopo wa Kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma wamepewa Mafunzo yatakayodumu Kwa siku mbili( Oktoba 9 na 10 , 2024) yatakayowajengea uwezo wa kusimamia utoaji wa Mikopo ya 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Walemavu.
Wakiongozwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri Bi. Joyce Mtui amesema lengo Kuu la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Wataalamu ambao wataenda kutoa Elimu na hamasa kwa Jamii juu ya uundaji Vikundi vyenye sifa ya kupata huduma hiyo ya Mikopo lakini pia kusimamia marejesho ya Mikopo hiyo.
Baada ya Mafunzo haya, Wataalamu hawa wataenda kufanya mikutano katika Kata zao kuhamasisha Jamii kuanzisha Vikundi vitakavyoweza kunufaika na Mikopo ya 10% ya mapato ya Halmashauri Kwa makundi haya ya Wanawake, Vijana na Walemavu.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa