Jumatano 5, September 2018.
Musoma, Mara.
Miradi sita ya Maendeleo yenye thamani ya Shillingi billioni 1.3 imekidhi viwango na kuzinduliwa sambamba na kuwekewa mawe ya msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Miradi hiyo imezinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mhandisi Charles Fransis Kabeho, leo Jumatano 5, September 2018 wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea katika Halmashauri hiyo.
Kati ya miradi hiyo sita mitatu ilizinduliwa ambayo ni Kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeti kilichopo Kata ya Nyambono chenye thamani ya shillingi 85,000,000 na ujenzi wa darasa shule ya Sekondari Nyambono iliyopo Kata ya Nyambono wenye thamani ya shillingi 14,785,900 na Ujenzi wa Zahanati ya Kigera Etuma iliyopo Kata ya Nyakatende wenye thamani ya shillingi 111,325,200.
Miradi mitatu iliwekwa mawe ya msingi ambayo ni mradi wa maji Sukuti - Kusenyi uliopo Kata ya Suguti wenye thamani ya shillingi 1,008,544,053 na ujenzi wa vyumba vya maabara shule ya Sekondari ya Mugango iliyopo Kata ya Mugango wenye thamani ya shillingi 64,416,202.40 na ujenzi wa nyumba ya mtumishi zahanati ya Kigera Ituma iliyopo Kata ya Nyakatende wenye thamani ya shillingi 26,049,000.
Jumla ya thamani ya miradi yote sita ni shillingi 1,308,120,355.40
Imetolewa na
Kitengo cha habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa