Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imeukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama.
Zoezi hilo la makabidhiano limefanyika leo Alhamisi 6, September 2018 katika uwanja wa mpira wa miguu wa Kamgego uliopo Katika Kata ya Kamgego Wilaya ya Butiama.
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma uliupokea Mwenge wa Uhuru jana Jumatano 5, September kutoka Halmashauri ya Mji Bunda.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ulizindua na kuweka mawe ya Msingi katika miradi sita ya Maendeleo yenye thamani ya Shillingi billioni 1.3
Miradi yote sita ya Maendeleo imekidhi viwango vya mbio za Mwenge Kitaifa vya ujenzi bora na gharama nafuu.
Imetolewa na
Kitengo cha habari na uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa