"Nilazima tufuatilie kwa umakini kile ambacho kimefundishwa hapa katika mafunzo haya na kuwasaidia walimu wengine ambao hawakufika katika mafunzo haya.Ninyi ni 50 tu ila kuna walimu wengi ambao hawakufika hapa hivyo niwasihi mkawe mabalozi kwa walimu wengine ambao hawakufika hapa". Kaimu RAS Mkoa wa Mara Ndg.Mkwasa Bulenga ameyasema hayo leo Septemba 7, 2023 katika mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu mahiri wa somo la Hisabati katika viwanja vya Shule ya Msingi Majita B.
Amesema pia kutokana na kutofuatilia kile ambacho mlifundishwa vyuoni inapelekea kufeli katika shule zetu.Hamtoi mazoezi ya kutosha na hata kama mkitoa hamfanyi masahihisho Pamoja na kufuatilia wanafunzi katika maendeleo yao.Niwaombe mkafanyie kazi mambo yote mliyofundishwa na pia mkawe mabalozi kwa wengine wapate ujuzi huu mlioupata hapa.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa