Leo tarehe 14 Januari, 2026, Timu ya Wataalam kutoka Mkoani imefanya kikao cha ufunguzi (Entrance Meeting) kwa ajili ya Ufuatiliaji wa Miradi, kikao kilichowakutanisha wataalam hao na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Baada ya kikao hicho muhimu, timu imeanza kutembelea miradi mbalimbali ili kujionea hatua za utekelezaji, ubora wa kazi na thamani ya fedha (Value for Money), pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam kwa ajili ya kuboresha zaidi utekelezaji wa miradi kwa manufaa ya wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma inaendelea kusimamia kwa karibu miradi ya maendeleo kwa uwazi, uwajibikaji na tija, ikilenga kuboresha huduma kwa wananchi na kuharakisha maendeleo endelevu.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa