Watumishi wa umma kutoka vitengo na idara mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma leo wamejitokeza kushiriki mazoezi ya pamoja ya mwili yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Suguti.
Mazoezi haya, yaliyohusisha jogging na mazoezi ya viungo, yameandaliwa kwa lengo la kuimarisha afya ya watumishi, kuongeza hamasa ya utendaji kazi, na kujenga mshikamano baina ya watumishi wote. yenye kaulimbiu isemayo “Mazoezi ni Afya – Jenga Mwili Wako kwa Kufanya Mazoezi.”
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma itaendelea kuratibu mazoezi ya aina hii mara kwa mara ili kuhakikisha watumishi wake wanadumisha afya bora, hali ambayo inachangia kuongeza ufanisi kazini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Ndg. Msongela Nitu Palela ameukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma Ndg. Bosco Ndunguru katika viwanja vya Chuo cha maendeleo ya jamii Buhare
Mwenge wa Uhuru 2025 leo 16 Agosti 2025 umepokelewa Wilayani Musoma.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Juma Chikoka akiupokea Mwenge wa Uhuru leo Agosti 16,2025 katika viwanja vya shule ya Msingi Kaburabura kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Aswege Enock Kaminyonge baada ya kuhitimisha mbio zake Wilayani Bunda katika Halmashauri ya Manispaa ya Bunda.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Suguti - Kwikonero, Barabara ya Majita) | 31117 - MUSOMA.
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa